Tetesi za soka Alhamisi: Al Hilal yakaribia kumsajili Watkins

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Al Hilal imefikia makubaliano ya takriban pauni milioni 50 na Aston Villa kumsajili mshambuliaji wa England, Ollie Watkins, mwenye umri wa miaka 30. (Fabrizio Romano)

Chelsea inamuwania kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, mwenye miaka 23, kama mbadala wa Enzo Fernandez, ambaye huenda akahamia Manchester City.Manchester City. (Sun)

Mshambuliaji wa Aston Villa anayelengwa, Rafael Leao, anakaribia kujiunga na Galatasaray kutoka AC Milan. Klabu hiyo ya Uturuki iko tayari kulipa takriban pauni milioni 38 kumsajili winga huyo wa Portugal mwenye miaka 27. (Corriere dello Sport - in Italian)

Sunderland imewasilisha ofa kwa Manchester City ya kumsajili kwa mkopo winga wa England, Jack Grealish, mwenye miaka 30. (Athletic - subscription required)

Chelsea pia inakaribia kukamilisha dili la pauni milioni 36 kumsajili beki wa Italia, Honest Ahanor, mwenye miaka 18, kutoka Atalanta. (Sky Sport Italy - in Italian, external)

Beki wa Barcelona na Spain, Alejandro Balde, mwenye miaka 22, bado yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Manchester United kuimarisha nafasi ya beki wa kushoto. (Fichajes - in Spanish)

Newcastle bado haijakata tamaa katika juhudi za kumsajili winga wa Lille na Belgium, Matias Fernandez Pardo, mwenye miaka 21, lakini haitaki kufanya uamuzi wowote unaoweza kukiuka kanuni za matumizi ya fedha za Ligi Kuu England na UEFA. (Mail - subscription required)

Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na France, Martin Terrier, mwenye miaka 29, analengwa na klabu yake ya zamani Lille kama mbadala wa Fernandez Pardo. (L'Equipe - in French), external

Fiorentina imekataa ofa ya awali ya pauni milioni sita kutoka Nottingham Forest kwa ajili ya beki wake wa kulia wa Brazil, Dodo, mwenye miaka 27. (Sky Sport Italy - in Italian, external)

Marseille inaamini itafanikiwa kumbakiza mshambuliaji wa Brazil, Igor Paixao, mwenye miaka 26, licha ya kuvutiwa naye na Arsenal pamoja na Sunderland. (Teamtalk)

Aston Villa imeanza kuulizia uwezekano wa kumsajili beki wa West Ham na France, Jean Clair Todibo, mwenye miaka 26, huku ikiendelea kutafuta beki wa kati. (Mail)

Kiungo wa Bayer Leverkusen na Argentina, Exequiel Palacios, mwenye miaka 27, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 23.5 kwenda Ipswich Town. (Sky Sports)

Everton inapanga kumsajili mshambuliaji wa Guinea Bissau, Franculino, mwenye miaka 22, kutoka Midtjylland. Klabu hiyo pia iko tayari kumuuza beki wa Republic of Ireland, Jake O'Brien, mwenye miaka 25.