BBC News, Swahili - Habari
Habari Kuu
Wahouthi 'wadhibiti' kisiwa cha kimkakati kwenye njia muhimu ya meli duniani
Waasi wa Houthi wamedhibiti Kisiwa cha Perim katika Mlango-bahari wa Bab al-Mandab, kulingana na chanzo cha habari.
Lissu hakuandaa mkutano uliomtia matatani - Heche
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche anaendelea kutoa ushahidi wake akiulizwa maswali na Lissu
Je, Korea Kusini inatuma wanajeshi katika Mlango wa Hormuz?
Ndege za doria za baharini aina ya P-8A Poseidon, meli za kutoa msaada na usambazaji pamoja na vikosi vya kutegua mabomu ni miongoni mwa chaguo zinazoweza kutumwa.
Siri ya mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani
Ethel Caterham, mwenye miaka 117, ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani aliye hai. Makala haya yanaangazia maisha yake pamoja na watu wengine waliowahi kushikilia rekodi hiyo, akiwemo Jeanne Louise Calment aliyefikisha miaka 122.
Mtanzania Clara Luvanga avunja rekodi ya usajili wa soka la wanawake duniani?
Mshambuliaji wa Tanzania Clara Luvanga amejiunga na Washington Spirit akitokea klabu ya Saudi Arabia, Al-Nassr, katika usajili unaoaminika kuwa miongoni mwa usajili wenye gharama kubwa zaidi katika historia ya soka la wanawake.
Je, Trump ataweza kumpa kila Mmarekani dola 5,000 alizoahidi?
Wachambuzi wanahoji iwapo ofa ya mwaka wa uchaguzi iliyotolewa na rais wa Marekani inaweza kutekelezeka, ni halali au inawezekana kumudu gharama zake.
Video mpya zafichua siri kuhusu Msaudi anayehusishwa na shambulio la 9/11
Picha hizi ni sehemu ya kesi ya kisheria iliyofunguliwa na familia za waathirika wa mashambulizi ya 9/11 dhidi ya Saudi Arabia, na hazijawahi kuwekwa hadharani hapo awali.
Kwa nini Mahakama haikuwaita Samia, Majaliwa na Mpango kutoa ushahidi?
Mahakama imeeleza kuwa si sahihi kuwaita mashahidi hao kwa madhumuni ya kuthibitisha iwapo walitishika au hawakutishika kutokana na kauli zinazolalamikiwa katika shauri hilo.
Kaijage aachiwa huru, kuripoti kwa RCO mwaka mmoja
Kabla ya kuachiwa huru, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Dodoma aliomba Kaijage aelekezwe kuwa na tabia njema.
Uteuzi wa mwanahabari kuwa mfalme baada ya kifo cha Oyo wazua mzozo Uganda
Anatarajiwa kutawazwa wiki hii, kabla ya mazishi ya Mfalme Oyo yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi
Unataka kupunguza gharama za data?
Soma mtandao wetu wa maandishi kwa gharama ndogo za data.
Gumzo mitandaoni
'Wizi wa nyeti': Jinsi mitandao ya kijamii ilivyochochea uvumi uliogeuka mauaji
Zaidi ya watu 80 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi ya umati, uchunguzi wa BBC umebaini baada ya kukusanya takwimu kutoka mataifa sita barani Afrika.
Nchimbi kufuata nyayo za Maalim Seif au kina Lowassa?
Katika historia ya siasa za Tanzania, wanasiasa waliowahi kuwa na nafasi kubwa ndani ya CCM lakini wakaondoka au kuondolewa wamewahi kuchukua njia tofauti kuhusu siasa na mustakabali wao kwenye nafasi za kisiasa. Nchimbi atachagua njia ipi?
Ndejembi kumrithi Nchimbi, ni mwanasiasa wa aina gani?
Iwapo atathibitishwa kwa mujibu wa taratibu za kikatiba, Ndejembi mwenye umri wa miaka 43 atachukua nafasi iliyoachwa na Nchimbi, ambaye alijiuzulu baada ya kuitumikia kwa takriban miezi 10.
Vigogo watano wa CCM waliioondoka katika nyadhifa zao chini ya Rais Samia
Tangu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, kuna wanasiasa kadhaa cha Chama cha Mapinduzi (CCM), ambao wameondoka kwa hiari au kwa shinikizo katika nafasi zao.
Tundu Lissu: Kuwa na kesi ya kujibu maana yake nini?
Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa uamuzi kuhusu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Tundu Lissu, kwamba ana kesi ya kujibu katika shtaka la uhaini linalomkabili. Hatua hii ina maanisha nini?
'Ninafanya kazi ya kuwabebea wengine ujauzito'
Lorna Fidelia hufanya kazi ya kuwabebea wengine uja uzito. Amewahi kubeba mimba ya pacha watatu miaka michache iliyopita na sasa anatafuta kubeba mtoto mwingine.
Je, Iran itaishambulia Ulaya?
Iran inaweza kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani barani Ulaya iwapo Donald Trump ataishambulia Iran tena, gazeti la Financial Times linaripoti.
Nani anafadhili magenge ya wahuni kuchochea ghasia za kisiasa Kenya?
Polisi nchini Kenya wamewakamata watu 37 wanaoshukiwa kuhusika na ghasia za kisiasa, baada ya kukutwa na silaha mbalimbali katika kaunti za Kisumu na Homa Bay. Ni nani yuko nyuma ya makundi haya ya vijana?
Je, Tanzania inaweza kufikia maridhiano ya kisiasa bila CHADEMA na Lissu?
Historia ya Tanzania inaonesha baadhi ya hatua kubwa za maridhiano ya kisiasa zilihitaji serikali na vyama vikuu vya upinzani kukaa meza moja.
Jinsi ubongo wa nzi unavyoweza kuelezea tabia ya binadamu
Watafiti walichora miunganisho milioni 124 kati ya seli zote za neva katika ubongo wa nzi dume.
Hatari 5 zinazoitishia dunia 2026
Licha ya Afrika kuchangia kwa kiwango kidogo katika mabadiliko ya tabianchi, bado ni miongoni mwa maeneo ambayo hayajajitayarisha vya kutosha kukabiliana na madhara yake ya moja kwa moja.
Viumbe 10 hatari zaidi duniani
Ingawa viumbe wengi wanajulikana kwa kuwatisha watu, ni mmoja tu anayeshikilia nafasi ya kuwa hatari zaidi. Hasa zaidi, kiumbe huyu ndiye anayesababisha vifo vya watu wengi zaidi.
BBC News Swahili sasa ipo WhatsApp
Dira ya Dunia TV
Kipindi cha habari motomoto, kinachowaweka watazamaji karibu zaidi na yanayojiri duniani























































