BBC News, Swahili - Habari
Habari Kuu
Moja kwa moja, Vyama vya upinzani Namibia vyapinga uteuzi wa jaji kwenye tume ya uchunguzi Tanzania
Vyama vya Affirmative Repositioning (AR) na Independent Patriots for Change (IPC) vimesema uteuzi huo unaweza kuibua maswali kuhusu uhuru wa mahakama ya Namibia na nafasi ya nchi hiyo katika mjadala kuhusu haki za binadamu nchini Tanzania.
Majaji wa Uganda, Namibia kuchunguza wahusika wa ghasia za Oktoba 29 Tanzania
Majaji wawili kutoka Uganda na Namibia ni miongoni mwa makamishna sita watakaochunguza waliohusika na makosa ya jinai na ukiukwaji wa sheria uliotokea kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi tume hiyo Ijumaa.
Watoto waliozaliwa wakati wa vita Sudan wanavyokosa utambulisho kisheria
Watoto wanaozaliwa kutokana na ubakaji mara nyingi hushindwa kupata cheti cha kuzaliwa, jambo linalowakabili na matatizo ya maisha yao yote.
Nani kumrithi Gianni Infantino ikiwa ataondoka FIFA?
Shinikizo linaendelea kuongezeka dhidi ya Rais wa FIFA, Gianni Infantino, lakini iwapo ataondoka madarakani, ni nani anayetarajiwa kuchukua nafasi yake?
Sekta 7 zinazotarajiwa kuzalisha ajira nyingi zaidi ifikapo 2030
Kwa mujibu wa ripoti ya Future of Jobs 2025 iliyochapishwa na World Economic Forum (WEF) mwezi Januari 2025, dunia inatarajiwa kuunda ajira mpya milioni 170 kati ya mwaka 2025 na 2030.
Vyakula 8 vinavyoweza kuzuia kiu
Wataalamu wa lishe wanaeleza kiasi halisi cha majimaji tunachohitaji na sababu zinazofanya vyakula viwe muhimu sawa na vinywaji.
Je, Saudi Arabia inanufaika na vita vya Iran?
Licha ya mzozo unaoendelea katika eneo la mashariki ya kati kutokana na vita Iran vilivyoathiri usafiri wa majini katika Ghuba ya Uajemi Saudia imepata faida kubwa kutokana na mauzo ya mafuta nje ya nchi.
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Juventus wafukuzia kumpata Zirkzee
Liverpool haina mpango wa kumfuatilia Djed Spence msimu huu wa joto, Juventus inataka kumsajili Joshua Zirkzee kwa mkopo, huku Arsenal na Manchester United zikiwatuma wasaka vipaji kumfualitilia Kaua Elias.
Viumbe 10 vyenye sura mbaya zaidi duniani
Watu wengi huvutiwa na wanyama wenye sura kama za watoto - fikiria macho makubwa, pua ndogo, nyuso za mviringo. Ni kwa sababu tunawajali watoto wetu.
Ukraine inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mifumo ya ulinzi wa anga
Mashambulizi ya makombora na droni yaliyofanywa na Urusi usiku wa kuamkia Jumatano dhidi ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, na maeneo yanayouzunguka yamesababisha vifo.
'Lango la Kuzimu la Turkmenistan:' Shimo linalowaka moto kwa miaka 40
Asili ya shimo hili inabishaniwa. Baadhi wanadai lilizuka miaka ya 1970 wakati mashine ya kuchimba gesi ya Kisovieti ilipotoboa gesi asilia chini ya ardhi kwa bahati mbaya; wengine wanaamini lilitokea tu wenyewe miaka ya 1960.
Unataka kupunguza gharama za data?
Soma mtandao wetu wa maandishi kwa gharama ndogo za data.
Gumzo mitandaoni
CHADEMA yakanusha kufanya mazungumzo ya siri na serikali
Julai 30, 2026, Rais Samia alikutana na viongozi wa vyama 18 kati ya 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu. CHADEMA hakikushiriki mkutano huo. Katika hotuba yake, Rais alisema; "Kuna mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari. Bado tunaendelea kupokea misukumo yake, conditions zake na matakwa yake,".
Kwanini kondo la nyuma linauzwa katika soko haramu?
Mwisho wa mwezi uliopita, mamlaka zilikamata kilo 500 za kile walichoamini kuwa ni kondo la nyuma la binadamu katika kituo haramu cha kuchakata bidhaa hizo mjini Islamabad, na kuwakamata watu watano.
Nchimbi awaambia Watanzania: "Pambaneni mpate Katiba mpya"
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi, amewataka Watanzania kuendelea kudai kupatikana kwa Katiba mpya yenye maridhiano ya kitaifa, akisema ndiyo msingi wa kuimarisha haki za binadamu, utawala bora na demokrasia nchini.
Jumuiya ya Madola yapendekeza kesi ya Tundu Lissu 'imalizwe' ndani ya siku 30
Jumuiya ya madola imeitaka serikali ya Tanzania kutafuta ufumbuzi wa kisiasa na kisheria kumaliza kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani nchni humo Tundu Lissu
Vyuo 10 bora Afrika Mashariki 2026
Elimu inasalia kuwa mojawapo ya vichocheo muhimu zaidi vya maendeleo kote Afrika, na Afrika Mashariki haijabaguliwa.
Kwa nini Kenya inapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa magenge ya wahuni?
Mwaka wa 2026 umeshuhudia visa vya kutisha vya uhuni ambavyo mpaka leo ni wachache ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kukabiliwa na mashtaka.
Ndege 10 bora za kivita duniani mwaka 2026
Toleo la ndege hizi ndio ishara moja ya nguvu ya ndege, kwa hivyo ndege za kivita za toleo la tano ndio zinaongoza kwa ubora, huku toleo la 4.5 zikifuata nyuma.
Je, Iran imedukua mifumo ya maji katika majimbo saba ya Marekani?
Japo Rais wa Marekani Donald Trump hajaelekeza kidole cha lawama kwa Iran, wataalamu wa masuala ya mtandao wameiambia BBC kwamba kuna uwezekano mkubwa shambulio hilo limeratibiwa na Tehran.
Ufahamu mtandao wa wauaji unaoajiri vijana kutekeleza mauaji Ulaya
Mtandao wa Foxtrot unaaminika kuhusika na takriban mauaji 35 barani Ulaya, na hutumia mbinu za "vurugu kama huduma", ambapo huajiri wengine kutekeleza mashambulizi au mauaji kwa niaba yao.
Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei yuko wapi?
Mojtaba Khamenei, ambaye alitangazwa kuteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, ndani ya wiki moja tangu kuuawa kwa baba yake, bado hajaonekana hadharani.
Kuna tofauti gani kati ya Freemason na Illuminati?
Illuminati ilianza kama "kundi la wasomaji" la siri la wanafunzi wa vyuo vikuu wanaopinga mafundisho ya kidini na waliojitolea kwa ugunduzi wa kisayansi.
BBC News Swahili sasa ipo WhatsApp
Dira ya Dunia TV
Kipindi cha habari motomoto, kinachowaweka watazamaji karibu zaidi na yanayojiri duniani























































