Kombe la Dunia 2026: Mshindi na timu zingine zinapata kiasi gani?

    • Author, Katharine Sharpe
    • Nafasi, BBC
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Pesa za zawadi zinazotolewa katika Kombe la Dunia la 2026 ni dola za kimarekani milioni 871 (£662m), n kiwango kikubwa kilichovunja rekodi.

Fifa ilitangaza zawadi ya pauni milioni 727 (£552m), ambayo ilikuwa ongezeko la 50% ya fedha zilizotolewa katika mashindano ya 2022 huko Qatar.

Lakini mwezi Aprili waliidhinisha ongezeko, kwa kuongeza zawadi ya ushiriki na ada ya maandalizi, na kuifikisha kwenye jumla hiyo mpya.

Pesa za zawadi zimegawanywa katika makundi mawili, zawadi kutokana na uchezaji na usaidizi wa kifedha.

Zawadi kutokana na utendaji

Kadiri timu zinavyoendelea katika mashindano hayo, ndivyo zinavyozidi kuzawadiwa kifedha. Fifa itatoa zawadi kwa timu zinazomaliza katika kila nafasi kama ifuatavyo. Pesa hizi ni katika dola za kimarekani:

  • Mshindi wa kwanza: dola milioni 51 (£38m)
  • Mshindi wa pili: milioni 34 (£25m)
  • Nafasi ya 3: milioni 30 (£22m)
  • Nafasi ya 4: milioni 28 (£20m)
  • Nafasi ya 5-8: dola milioni $20 (£14m)
  • Nafasi ya 9-16: milioni 16 (£11 milioni)
  • Nafasi ya 17-32: milioni 12 (£8m)
  • Nafasi ya 33-48: milioni 10 (£7m)

Malipo haya yatakuwa dola milioni 703 kati ya dola milioni 871, huku kiasi kilichobaki cha dola milioni 168m (£152m) zikilipwa miongoni mwa timu bila kujali uchezaji wao.

Zawadi zisizotegemea utendaji

Pesa zilizobaki zitagawiwa sawasawa kwa timu zote zinazoshiriki katika mfumo wa:

  • Pesa za maandalizi: dola milioni 2.5m kwa kila taifa
  • Michango ya ziada kwa timu: zaidi ya dola milioni 16

Hii ina maana kwamba kila timu itapata angalau dola milioni 12.5 kwa kushiriki katika mashindano hayo ikijumuishwa na ada ya kufuzu ya dola milioni 10.

Pesa za maandalizi ni kuchangia gharama kama vile kambi za mazoezi na usafiri kwa ajili ya timu kabla ya mashindano.

Fifa inaelezea 'michango ya ziada kwa timu' kama 'ruzuku kwa gharama za benchi la timu na mgao kwa tiketi za timu', kwa lengo la kupunguza tofauti za kifedha kati ya mataifa wakati wa kulipa gharama zinazohusiana na kucheza Kombe la Dunia, kama vile usafiri, vifaa na utawala.