Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Barcelona inamfukuzia Hincapie Arsenal

 Hincapie

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Barcelona inafikiria kumsajili beki wa Arsenal na Ecuador Piero Hincapie, 24. (Mail)

Beki wa Manchester City na Ureno Ruben Dias, 29, amemwagiza wakala wake kuanza mchakato wa uhamisho wake huku klabu za Paris St-Germain, Bayern Munich na Real Madrid zikimfuatilia. (Caught Offside)

Liverpool inashinikiza makubaliano ya haraka na winga wa RB Leipzig Yan Diomande, huku Paris St-Germain na Manchester City zikifuatilia kwa karibu hali hiyo na tayari zimefanya mazungumzo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19. (Florian Plettenberg)

Crystal Palace inataka kumshawishi kiungo wa England Adam Wharton, 22, na kiungo wa Japan Daichi Kamada, 29, kutoondoka kufuatia ushindi wao wa fainali ya Ligi ya Conference. (Sky Sports)

Bournemouth haina mpango wa kupokea ofa zozote za msimu wa joto kwa mshambuliaji wa Mfaransa Eli Junior Kroupi, 19, winga wa Brazil Rayan, 19, na kiungo wa kati wa Uingereza Alex Scott, 22, huku klabu kadhaa zikoonyesha nia ya kutakuwasajili wachezaji hao watatu. (Guardian)

Manchester United na Chelsea ni miongoni mwa klabu zinazofikiria kumsajili Scott katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Team Talk)

Mshambuliaji wa West Ham na Ujerumani Niclas Fullkrug anataka kuondoka baada ya klabu hiyo kushushwa daraja huku Werder Bremen ya Bundesliga ikiwa miongoni mwa wale wanaomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. (Sky, kwa Kijerumani)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sporting ya Ureno inataka kumsajili tena kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha mwenye umri wa miaka 30 wakati mkopo wake wa muda mrefu Tottenham kutoka Bayern Munich utakapomalizika. (A Bola, kwa Kireno)

Leeds United inajiandaa kuwasilisha dau la kumnunua kiungo wa kati wa Lyon mwenye umri wa miaka 24 na Merika Tanner Tessmann kama sehemu ya shughuli za usajili wa majira ya joto. (Football Insider)

Manchester City wanatathmini chagua lao ikiwa winga wa Brazil Savinho, 22, ambaye analengwa na Tottenham, ataamua kukihama klabu hicho. (Fabrizio Romano)