Jinsi Iran ilivyotaka kumuua mmoja wa wanangu – Netanyahu

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kuwa Iran ilijaribu kumuua mmoja wa wanawe, lakini hakutaja ni lini tukio hilo lilitokea.

Pia, Netanyahu hakusema ni yupi kati ya wanawe aliyelengwa katika jaribio hilo la mauaji wala jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Kauli ya Netanyahu inaakisi hali ya mvutano inayoendelea tangu kuzuka kwa vita kati ya Iran na Marekani mwezi Februari, vita vilivyosababisha kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na viongozi wengine wa Iran.

Waziri Mkuu huyo wa Israel, ambaye muungano wake unakabiliwa na changamoto ya kupungua kwa umaarufu, alitoa madai hayo miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika Oktoba 27, wakati wa mahojiano ya simu na kituo cha televisheni cha Israel, Channel 14.

Aliatoa kauli hiyo akijibu taarifa kwamba vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimekataa kumpatia ulinzi mwanasiasa wa upinzani nchini humo.

"Najua kuna mambo ya kushangaza kuhusu watoto wangu, lakini ndivyo ilivyo. Iran ilimshambulia mmoja wa watoto wangu. Iran ilitaka kumuua mmoja wa watoto wangu," Netanyahu aliambia kituo cha televisheni kinachounga mkono serikali.

"Kwa hivyo, hali ya usalama inatia wasiwasi," alisema, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Ubalozi wa Marekani mjini New York haukujibu ombi la ufafanuzi zaidi kuhusu madai hayo.

Netanyahu pia alisema alimwambia mkuu wa shirika la usalama la Shin Bet, David Zini, kwamba ulinzi wa kutosha unapaswa kutolewa kwa yeyote anayewania wadhifa wa Waziri Mkuu.

Vyombo vya habari vya Israel hapo awali viliripoti kuwa Zini alikataa kutoa ulinzi kwa Gadi Eisenkot, akiiambia tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuwa hakukuwa na tishio la kiusalama dhidi yake.

Inatabiriwa kuwa chama cha Eisenkot kitashinda viti vingi katika uchaguzi ujao, ingawa serikali nchini Israel kwa kawaida huundwa kupitia ushirikiano wa vyama badala ya chama kimoja kupata wingi wa viti.

Marekani imetangaza mfululizo wa vikwazo dhidi ya Iran na kutishia kuchukua hatua dhidi ya nchi zilizosaidia Iran.

Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, alielezea hatua hiyo kuwa "shambulio baya zaidi la kiuchumi katika historia."

Bessent, ambaye alitaja hali hiyo kuwa "janga la kiuchumi" kwa Iran, alisema Marekani itakata uhusiano wote wa kiuchumi na Iran, na kuongeza kuwa nchi yoyote itakayofanya biashara na Iran nayo itatengwa.

Hata hivyo, Waziri wa Uchumi wa Iran, Ali Madanizadeh, alisema kuwa Iran inapanga kuendeleza vikwazo hivyo kwa miaka miwili, na itaendelea kuipinga Marekani.

Vita hivyo vimesababisha kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta ghafi katika masoko ya dunia, na Iran imetishia tena kuchukua hatua zaidi za kuzuia usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka eneo hilo.

Iran pia imetoa tishio jipya dhidi ya meli yoyote itakayojaribu kupita katika Lango la Bahari la Hormuz bila idhini yake.

Benjamin Netanyahu ni nani?

Benjamin Netanyahu amekuwa kiongozi wa nne wa taifa kutolewa hati ya kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Benjamin Netanyahu alizaliwa Tel Aviv mwaka 1949. Familia yake ilihamia Marekani mwaka 1963 baada ya baba yake, Benzion, mwanahistoria mashuhuri na mtetezi wa kuanzishwa kwa taifa la Wayahudi, kupata kazi ya kufundisha huko.

Akiwa na umri wa miaka 18, alirejea Israel na kujiunga na jeshi, ambapo alitumikia kwa miaka mitano na kufikia cheo cha kapteni katika kikosi cha kupambana na vifaru kilichoitwa Sayeret Matkal.

Alikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa katika shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Ubelgiji lililofanywa na wapiganaji wa Kipalestina; wapiganaji hao waliteka ndege hiyo, na yeye mwenyewe alipigana katika Vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1973.

Mwaka 1976, kaka yake Netanyahu, Jonathan, aliuawa wakati akiongoza operesheni ya kuwaokoa raia wa Israel waliokuwa kwenye ndege iliyokuwa imeelekezwa kwa nguvu nchini Uganda. Kifo chake kiliongeza umaarufu wa familia ya Netanyahu, huku jina lake likiwa gumzo kubwa kitaifa.

Netanyahu alianzisha Kituo cha Kupambana na Ugaidi kwa ajili ya kumuenzi kaka yake, na mwaka 1982 akawa naibu balozi wa Israel nchini Marekani.

Netanyahu alijipatia umaarufu mkubwa ghafla nchini Israel. Alikuwa hodari wa kuiga lafudhi za Kiingereza na Kimarekani, akionekana katika vipindi vya televisheni vya Marekani, na alijulikana kama mtetezi imara wa Israel.

Aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Israel katika Umoja wa Mataifa mwaka 1984.